 |
| Jonas Mkude kiungo wa Simba SC |
 |
| Awadhi Juma kiungo mshambuliaji wa simba |
 |
| Awadhi Juma. |
 |
| Jonas Mkude akichuana na mchezaji wa mbeya Sity. |
 |
| Said Ndemla akiwa kazini. |
 |
| Ndemla |
 |
| Emmanuel Okwi Simab Sc. |
 |
| Emmanuel Okwi akimhadaa kipa wa Yanga. |
 |
| Add caption |
 |
| Okwi Vs Azam |
 |
| Ramadhani Singano'Messi' kazini. |
SIMBA sasa imekamilika na kiungo, Jonas Mkude, yupo tayari kupangwa na kiungo mwingine yeyote kwenye kikosi cha timu hiyo ili kuiletea timu mafanikio kwani wachezaji wote wapo kwenye kiwango cha juu kuweza kuipatia timu ushindi.
Ikiwa chini ya Kocha Patrick Phiri, Simba ipo kambini Zanzibar inakojiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Desemba 26 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkude aliliambia Mwanaspoti ana imani sasa kikosi chao kimekamilika na kila mchezaji yupo kwenye kiwango cha juu na anaweza kuisaidia timu kupata matokeo mazuri.
Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji wachache waliojihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba hivyo kazi kubwa kwa Phiri ni kumtafutia kombinesheni na kiungo mwingine kwenye nafasi hiyo.
Mara kadhaa Phiri amekuwa akiwatumia Mkude na Shaaban Kisiga katikati pia mara nyingine amekuwa akimpanga na Said Ndemla au Awadh Juma kulingana na mfumo anaoutumia.
“Timu yetu ipo vizuri kwa sasa, kikosi kimekamilika, binafsi sina tatizo la kucheza na kiungo mwingine yeyote kwenye nafasi ya kati, nipo tayari kutengeneza kombinesheni na kiungo mwingine atakayepangwa na kocha, wote wapo vizuri,” alisema Mkude
Akizungumzia maandalizi kuelekea mechi yao na Kagera Sugar, Mkude alisema wanajindaa vizuri kushinda ili kurejesha imani kwa wapenzi wa timu hiyo licha ya Kagera kuwa ni timu nzuri na anategemea italeta upinzani kwenye mchezo huo.
“Kagera ni timu nzuri lakini sisi tumejiandaa vizuri, tuna faida pia ya kucheza nyumbani kwani Kagera ukicheza nayo kwao mechi huwa ngumu zaidi,” alisema Mkude.
Hadi sasa Simba ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi tisa baada ya kucheza mechi saba na kutoka sare sita huku ikiambulia ushindi mara moja.
0 comments:
Post a Comment