![]() |
| Uongozi mpya wa timu ya Polisi Morogoro |
Pia alimtangaza Odilo Tweve kuwa Makamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe ambao ni Paul Simkoko na Harry Mwambene (si waajiriwa wa Polisi). Pia aliwatangaza wajumbe ambao ni askari kuwa ni Natali Bruno, Ramadhani Fumo na Kabunga Jindibu na kwamba baada ya kuchaguliwa viongozi hao wapya watateua Katibu, Mwekahazina, Msemaji pamoja na Kamati ya Saidia Polisi Morogoro Ishinde.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo mwakilishi wa TFF, Jonas Mahanga, aliwataka viongozi hao wapya kutoendeleza makundi yaliyokuwepo wakati wa kampeni badala yake waiongoze timu hiyo kwa kufuata katiba na kanuni.
Naye mlezi wa timu hiyo ambaye ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, aliwataka viongozi hao watakaokaa madarakani kwa miaka minne kudumisha uwazi katika utawala.
Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya, Chembera aliahidi kuendeleza mipango mizuri iliyoanzishwa na uongozi uliotangulia.


0 comments:
Post a Comment