YANGA MIKONONI MWA BDF IX YA BOTSWANA CAF.

12/23/2014 03:35:00 pm
BDF IX, moja ya kati mechi za ligi (Nyekundu na Kijani)


BDF IX, wapo nafasi ya pili katika ligi ya Botswana.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Azam FC imepangwa kucheza na El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikipangiwa kuanza na Botswana Defence Force (BDF) ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana Jumatatu na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Azam na Yanga zote zitaanza kucheza mechi zao nyumbani kati ya Februari 13 na 15 kisha kurudiana kati ya Februari 27 na Machi Mosi mwakani.

Azam itakutana na El Merreikh ambayo ni klabu bingwa ya Sudan na pia ni bingwa mtetezi wa Kombe la Kagame wakati Yanga itakuwa na kibarua na BDF inayomilikiwa na Jeshi la Botswana.

Yanga imepata nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho baada ya kushika nafasi ya pili katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara ambapo Azam ilitwaa ubingwa na kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.

Polisi ya Zanzibar itacheza na CF Mounana ya Gabon katika Kombe la Shirikisho huku KMKM ikipangiwa kucheza na Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 comments:

Post a Comment