SELEMAN MATOLA kocha msaidizi wa Simba SC juzi usiku alijikuta akilalama baada ya timu hiyo kuchezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.
Kutokana na hali hiyo, Matola aliwashushia lawama wachezaji wa kimataifa timu hiyo kutoka Uganda ambao hawakuambatana na kikosi hicho visiwani hapa kwa ajili kushiriki Mashindano ya Mapinduzi yalioanza juzi Alhamisi.
Waganda hao ni Emmanuel Okwi, Simon Sserunkuma, Juuko Mrushid na Joseph Owino ambao kwa pamoja hawakuweza kuambatana na kikosi hicho kutokana wote kudaiwa kuwa kwao nchini Uganda.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Matola alisema kuwa kikosi chake kimeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na kukosekana kwa nyota hao.
“Kukosekana kwa wachezaji wa kimataifa ndiyo hasa kumesababisha tupate matokeo haya kwa sababu nimelazimika kuchezesha wachezaji wasiokuwa na uzoefu wa mashindano, hivyo nadhani jambo hili viongozi watakuwa wameliona na watalifanyia kazi,” alisema Matola.
Kwa miaka ya hivi karibuni wachezaji kutoka Uganda wametokea kutokuwa na nidhamu ya kazi yao, siku zote huchelewa kuripoti kambini ukilinganisha na wachezaji wa kutoka nchi nyingine. Kwa ushauri kwa vilabu vya Tanzania kuachana na wachezaji wa Kiganda na waweze kuangalia upande mwingine kwani wamekuwa kero kwa vilabu na mashabiki.

0 comments:
Post a Comment