![]() |
| Beno Njovu aliyekuwa Katibu wa Yanga SC. |
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amefunguliwa mashitaka ya madai ya ubadhirifu wa fedha katika timu hiyo kongwe hapa nchini.
Inasemekana Njovu na ofisa mwingine wa masuala ya fedha aitwaye Rose ndiyo watuhumiwa, Lakini bado uongozi wa Yanga haujaweka wazi kuhusiana na suala hilo.
Imfahamika tayari mashitaka hayo yamefunguliwa na Rose alishikiliwa na sasa yuko nje kwa dhamana.
Hata hivyo, uongozi wa Yanga umeshindwa kuweka wazi ubadhirifu hasa ni upi kwa kuwa Njovu hakuwa amekabidhi ofisi.
Chanzo kinaeleza kama wahusika hao wangekuwa wamekabidhi ofisi, huenda ingekuwa ni rahisi kujua kama kuna upungufu.

0 comments:
Post a Comment