Paul Kiongera ametua nchini Jumamosi iliyopita akitokea nchini India alipokwenda kufanyiwa upasuaji wa goti na anatarajia kwenda mapumziko nyumbani kwao Kenya.Kiongera alikwenda India mwanzoni mwa mwezi huu kufanyiwa upasuaji wa goti ambalo lilimsumbua kwa muda mrefu.
Akizungumza Katibu wa Simba, Stephen Ally alisema kuwa Kiongera, ametua nchini siku ya Jumamosi jioni na hali yake inaendelea vizuri.
“Kwa sasa tunasubiri ripoti kutoka kwa daktari kuona inasemaje juu ya hali yake, lakini lengo la Simba ni kumuacha hadi atakapokuwa fiti kabisa ndipo aweze kuitumikia timu hii tena.
“Ameshaanza mazoezi mepesi ya kuimarisha kiwango chake anatarajia kuondoka nchini wakati wowote kuelekea Kenya kwa ajili ya mapumziko,” alisema Stephen.Kiongera alisajiliwa na Simba akitokea KCB ya nchini Kenya, lakini alifanikiwa kuitumikia kwenye mchezo mmoja tu kabla hajaumia na kukaa nje kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Simba ilishajaza nafasi yake kwa kumsajili mchezaji mwingine wa kimataifa kutoka Uganda, Dan Sserunkuma.

0 comments:
Post a Comment