Katika mazoezi hayo yaliyosimamiwa na kocha, Patrick Phiri, pamoja na msaidizi wake, Selemani Matola, yalidumu kwa saa mbili ambapo mazoezi hayo yalihudhuriwa na wachezaji 18 tu, ambapo kati yao ni mchezaji mmoja tu wa kigeni aliyekuwepo uwanjani hapo ambaye ni, Danny Sserunkuma.
Ofisa Habari wa Simba, Humprey Nyasio, alisema kuwa anajua alipo Emmanuel Okwi tu lakini wengine hana taarifa zao. Ila taarifa zilizopo mchezaji Emmanuel Okwi amerejea Uganda kwa ajili ya kumalizia mambo yake ya fungate baada ya kufunga ndoa wiki iliyopita.
Katika hatua nyingine, Nyasio aliongezea kwa kusema kuwa kikosi hicho kinatarajia kwenda Visiwani Zanzibar, leo kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya michezo ya ligi na kujiweka sawa kabla ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambayo yanatarajiwa kuanza kesho.
“Leo Jumatano tunatarajia kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi yetu ya kujiandaa na michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara pia kujiweka sawa kabla ya kushiriki Mashindano ya Kombe la Mapinduzi,” alisema Nyasio.

0 comments:
Post a Comment