Kombe hilo la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari Mosi, mwaka huu michuano inayoshirikisha pia timu za Simba, Yanga, Mtibwa na Azam pia kutoka Tanzania Bara.Yanga, mwaka jana ilizuia timu yao kwenda Zanzibar kushiriki michuano hiyo kwa sababu tofauti huku ikitaka kupeleka kikosi chao cha vijana cha U20.
Akizungumza makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Clement Sanga, alisema kikosi chao kinaendelea na mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kujiwinda na michuano hiyo.
Sanga alisema timu yao inatarajiwa kuelekea Zanzibar, kesho ikiwa na kikosi kamili kitakachoongozwa na Kocha Mkuu Mholanzi, Hans van Pluijm.“Tumekubaliana viongozi wote na benchi la ufundi kuipeleka timu Zanzibar kwa ajili ya kwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi.
“Hivyo timu inaendelea kujifua kujiandaa na michuano hiyo, tumepanga kukipeleka kikosi kizima kwenye michuano hii katika kuhakikisha tunachukua ubingwa,” alisema Sanga.Kwa upande wa Simba wenyewe wamepanga kuondoka leo kwenda kwenye michuano hiyo, hii inamaana kuwa ratiba ya Ligi Kuu Bara sasa itakuwa imebadilika kwa baadhi ya michezo.

0 comments:
Post a Comment