MTIBWA SUGAR YAIPANIA AZAM FC.

12/31/2014 09:24:00 pm
Mtibwa Sugar.
Kutokana na kikosi cha Mtibwa Sugar kuimarika zaidi, uongozi wa klabu hiyo umesema hautakuwa tayari kuipa nafasi Azam FC kuuchukua ubingwa mbele yao.

Timu hizo zitakutana wikiendi hii, kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, alisema maendeleo ya kikosi chake yako vizuri na anaamini kombinesheni ya wachezaji alionao itafanya vizuri.
Azam FC.

“Mpira hauongelewi kwa mdomo bali miguu pekee ndiyo inayoongea uwanjani, hivyo wadau wajitokeze kwa wingi kuona mafanikio ya Mtibwa msimu huu yanavyoendelea kusonga mbele.

“Wachezaji wako vizuri, bado tunaendelea na mazoezi yetu ya kujiweka vizuri zaidi kuhakikisha tunafanya poa msimu huu, kwani lengo kubwa ni kuchukua ubingwa ambao upo mikononi mwa Azam na siyo vinginevyo,” alisema Maxime.

0 comments:

Post a Comment