MAJANGA YANGA:TAMBWE AUUMIA MAZOEZINI.

12/25/2014 06:20:00 pm
HABARI KAMILI: Mshambuliaji mpya wa Yanga, Amissi Tambwe ameumia nyama za paja.

Tambwe ameumia wakati wa mazoezi ya Yanga yaliyofanyika katika Uwanja wa Boko jijini Dar, jana baada ya kugongwa na beki Rajab Zahir.

Hali hiyo inaonyesha kuzua hofu kwamba kama Tambwe aliyejiunga na Yanga akitokea anaweza kurejea  uwanjani na kucheza dhidi ya Azam FC.

Yanga inaivaa Azam FC wikiendi hii katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na Tambwe ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kuongoza mashambulizi ya Yanga.

0 comments:

Post a Comment