MASHABIKI SIMBA WAKERWA NA MAKOSA YA IVO MAPUNDA.

12/27/2014 10:55:00 pm
Ivo Mapunda Kipa wa Simba SC.
Mashabiki wa Simba wamemshushia lawama za moja kwa moja kipa wao namba moja, Ivo Mapunda kutokana na kipigo cha kufungwa bao cha 1-0, walichopata kutoka kwa Kagera Sugar.

Mchezo huo wa raundi ya nane, ulipigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Baada ya mchezo huo, mashabiki walitoa lawama kwa Mapunda kuwa ndiye aliyechangia kufungisha bao hilo kutokana na kutokuwa makini langoni.

Lakini wakati mashabiki wakisema hivyo, kocha wa timu hiyo, Patrick Phiri alitoa lawama zake kwa washambuliaji wake kwa madai kuwa walishindwa kutumia nafasi nyingi walizopata.“Tumefungwa bao la kimichezo sina haja ya kutoa lawama kwa mtu, lakini safu ya ushambuliaji haikuwa makini na imepoteza nafasi nyingi za wazi,” alisema Phiri.

0 comments:

Post a Comment