RAJABU ZAHIRI AKABIDHIWA MIKOBA YA CANAVARRO KUIKABILI AZAM FC.

12/27/2014 11:09:00 pm

Rajab Zahir  Beki Yanga SC.
YANGA SC, kesho itashuka uwanja wa Taifa kumenyana na Azam FC katika mechi ya ligi kuu mznguko wa nane(8), lakini habari mbaya kwa wadau wa Yanga ni kumkosa nahodha na beki kisiki, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye anatumkia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata katika mechi yao na Kagera Sugar ambayo Yanga ililala bao 1-0, mjini Bukoba katika raundi ya saba.

Hata hivyo hofu kubwa kwa Yanga ni juu ya fowadi matata na mchezaji bora msimu uliopita, Kipre Tchetche ambaye ni tegemeo kwenye mashambulizi ya Azam FC.Licha ya Kocha Hans van Der Pluijm kukataa kuweka wazi ni mchezaji yupi ataziba pengo la Cannavaro kwenye mchezo huo, lakini imefahamika kuwa Rajab Zahir ndiye amepewa jukumu hilo la kumlinda Kipre Tchetche.

Katika mazoezi ya kikosi cha Yanga yaliyofanyika jana asubuhi kwenye Uwanja wa Boko, Ununio, Pluijm alikuwa ‘aki-dili’ sana na Zahir, lakini kadiri mazoezi yalivyokwenda alimjaribu, Edward Charles baada ya kumpanga sambamba na Kelvin Yondani ‘Cotton’ katika vikosi viwili alivyotengeneza mazoezini hapo.

Alipoulizwa Pluijm kuhusu mbadala alisema: “Suala hilo linabaki kuwa siri ya benchi la ufundi, si kila kitu lazima kiwekwe hadharani. Najua ni mchezo mgumu ninajaribu kuwajengea kujiamini wachezaji wote hivyo nitajua nani atacheza mchezo huo.”Wakati huohuo Pluijm anatarajia kumtumia kiungo Salum Telela kama kiungo mkabaji kwenye mechi dhidi ya Azam FC kesho.

0 comments:

Post a Comment