KATIBU YANGA ASAKWA NA POLISI.

12/27/2014 11:17:00 pm
Beno Njovu aliyekuwa katibu Yanga SC.
POLISI jijini Dar es Salaam linaendelea kumsaka aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu.
Habari za kipolisi kutoka ndani ya Jeshi hilo zimeeleza kwamba juhudi za kumtia nguvuni Njovu anayetuhumiwa kwa ubadhilifu zimekuwa zikiendelea kwa juhudi kubwa.

Lengo ni kumtia nguvuni ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili kuhusiana na ubadhirifu, vilevile
Mhazini wa Yanga aliishashikiliwa na jeshi hilo kabla ya kuachiwa kwa dhamana katika tuhuma zinazohusiana na jambo hilo.

0 comments:

Post a Comment