![]() |
| Amissi Tambwe Yanga SC. |
Nyota huyo wa zamani wa Vital’O, Black Eagle na Simba atalazimika kuwa nje wakati timu yake itakaposhuka dimbani kesho kumenyana na Azam ambao ni mchezo wake wa kwanza tangu atue Jangwani.
Mfungaji bora msimu uliopita, aliumia Jumatano ya wiki hii kwenye mazoezi baada ya kugongana na Rajab Zahir, ambapo hata jana alishindwa kufanya mazoezi na wenzake.Mbali na Tambwe, kiungo Hassan Dilunga alipata jeraha jana mazoezini, lakini daktari wa timu hiyo, Juma Sufian alikataa kulitolea ufafanuzi ni lini Tambwe atarejea ambapo alikataa katakata kuongea.

0 comments:
Post a Comment