TAMBWE NA SHERMAN WAGOMBEA NAMBA YANGA.

12/21/2014 02:27:00 pm

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Mliberia, Kpah Sherman.

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Mrundi, Amisi Tambwe.
WASHAMBULIAJI wapya wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe na Mliberia, Kpah Sherman, wameanza kuonyeshana mavituzi katika mazoezi ya timu hiyo.

Nyota hao wote walijiunga na kikosi hicho hivi karibuni katika usajili wa dirisha dogo, Tambwe yeye alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Sherman miaka miwili.

Katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Loyola, Mabibo jijini Dar washambuliaji hao kila mmoja ameonekana kuonyesha uwezo mkubwa kwa lengo la kujiwekea mazingira mazuri ya kushinda vita ya kuingia katika kikosi cha kwanza.

Wakiendelea na mazoezi hayo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Salvatory Edward aliyesaidiana na Shadrack Nsajigwa walitoa programu maalumu ya kushambulia.

0 comments:

Post a Comment