KOCHA GORAN KUPONOVIC AMKUBALI OKWI.

1/23/2015 04:04:00 pm
Emmanuel Simba SC.
KOCHA Mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic, amemsifia mshambuliaji wa timu yake, Emmanuel Okwi kutokana na kuonyesha nidhamu kwa muda wote aliokuwa naye lakini akamuonya kuwa anatakiwa kuendelea kuwa hivyo, kinyume na hapo hawataelewana.

Okwi ameanza kuwa chini ya kocha huyo hivi karibuni baada ya kutumia muda mwingi kuwa katika mambo ya familia wakati kocha huyo akianza kazi.Akizungumza na Championi Ijumaa, Kopunovic alisema kwa sasa anafurahishwa na tabia ya Okwi ambayo amekuwa akionyesha mazoezini, hali inayofanya ajisikie kuwa na amani muda wote.

“Sina tatizo kabisa na Okwi, kwani tangu ajiunge na kikosi hiki tulipokuwa Zanzibar kwenye Mapinduzi, amekuwa ni mtu safi na mwenye nidhamu ya hali ya juu.“Naomba aendelee hivyo kila siku kwa faida yake na ya timu,” alisema Kopunovic.

0 comments:

Post a Comment