YANGA SC. YAIFUATA POLISI MOROGORO KATIKA MCHEZO WA LIGI KUU, VPL.

1/23/2015 11:14:00 pm
KIKOSI cha Young Africa (Yanga), leo kimeelekea Mkoani Morogoro kuwavaa wenyeji wao Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi kuu utakao fanyika Kesho jumamosi tarehe 24/1/2015..
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Hans Van Der Pluijm, inaenda kuvaana na Polisi Morogoro ambao wamepanda ligi kuu mwaka huu huku, wakiwa wametoka kupata matokeo ya Sare dhidi ya Ruvu Shooting wiki jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam mchezo ambao uliandamwa na vurugu za hapa na pale.
Chanzo chetu kutoka Ndani ya uongozi wa Yanga ambae ameambatana na timu katika safari hiyo, amesema kikosi kizima cha Wanajangwani hao kipo vizuri kiafya kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kunako dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.

0 comments:

Post a Comment