Baada ya kupoteza mchezo kwa kufungwa goli 1-0 kutoka kwa Stand United ya Shinyanga, Simba imeamka toka usingizini na kuinyeshea mvua ya magoli timu ya Tanzania Prisons ‘Wajela jela’ wa Mbeya kwa kuiadhibu kwa goli 5-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa uwanja wa Taifa.
Ibrahim Hajib ameibuka nyota wa mchezo huo baada ya kukwamisha magoli matatu ‘hat-trick’ aliyo yafunga kipindi ha kwanza. Hajib alifunga goli la kwanza dakika ya 15 akimalizia pasi ya mshambuliaji wa Uganda, Dan Sserunkuma, akafunga goli la pili dakika ya 21 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Mohamed Yusuf na akakamilisha goli lake la tatu dakika ya 41 kwa mkwaju wa penati baada ya Lugano Mwangama kuunawa mpira kwenye eneo la hataei.
Simba wakionekana kutulia na kucheza mpira wa pasi nyingi fupifupi wakiongozwa na viungo wao waliocheza kwa ubora wa hali ya juu Said Ndemla na Jonas Mkude ambao muda wote wa mchezo walionekana kutawala eneo la katikati.
Kipindi cha pili samba waliendelea kuliandama lango la Prisons na mashambulizi yao ya mara kwa mara yalizaa matunda baada ya Emanuel Okwi kuifungia Simba bao la nne dakika ya 75 kwa shuti kali lililo mshinda mlinda mlngo wa Tanzania Prisons.
Ramdhani Singano akamalizia mvua ya magoli kwa kufunga goli la tano katika dakika ya 84 akimalizi pasi kutoka kwa Emanuel Okwi na kufanya matokeo yasomeke, Simba 5 na Tanzania Prisons wakiwa hawajapata kitu.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 23 baada ya kucheza mechi 16 huku ikiendelea kubaki kwenye nafasi ileile ya nne nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 24, wakati Azam wakiwa na pointi 27 na Yanga ikiwa kileleni kwa pointi 31.

0 comments:
Post a Comment