PRISONS WAAMKA, WAICHAPA STAND 3-0.

3/15/2015 11:27:00 am
PRISONS Mara baada ya kumtimua kocha wao David Mwamwaja, Prisons imeanza kuonyesha cheche baada ya kuipiga Stand United kwa mabao 3-0.

Stand iliyoonekana kuwa moto, leo imekiona cha moto katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mabao ya Prisons yalipachikwa na Laulian Mpalile, Hamis Maigo na Salum Kamenya aliyehitimisha kazi hiyo katika dakika ya 65..

JKT nayo imeendelea kufanya vizuri baada ya kuichapa Polisi Moro kwa bao 1-0.

Bao la Polisi limefungwa na beki Mohammed Faki katika dakika ya 75.

0 comments:

Post a Comment