![]() |
| Mbeya City |
Klabu hiyo msimu uliopita ilifanikiwa kuuza jezi kutokana na timu hiyo, kujizolea mashabiki wengi baada ya kuanza vyema ligi na kumaliza katika nafasi ya tatu lakini msimu huu inashika mkia kwenye ligi.
Katibu wa timu hiyo, Emmnuel Kimbe, amesema wameamua kufanya hivyo ili kupunguza ule upenyo wa jezi feki kuzagaa mitaani.
“ Tumezindua mpango wetu mpya wa uuzaji wa jezi na safari hii tumeleta na sweta ambazo shabiki popote pale alipo ndani au nje ya nchi ataweza kununua kwa njia ya mtandao akiwa na visa kadi ambayo ataitumia katika benki yoyote, jezi bei yake ni 20,000 na sweta 30,000.“Na hii tumefanya hivi kutokana na kupunguza lile wimbi la kuuza jezi ambazo sio halali,”alisema Kimbe.


0 comments:
Post a Comment