MBEYA CITY YAZINDUKA, YAMPIGA NDANDA FC BAO 1- 0.

12/29/2014 01:34:00 pm
Mbeya City
TIMU ya Mbeya City, imepata tabasamu baada ya muda mrefu kupita, hiyo ni kutokana na kuifunga Ndanda FC bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani hapa.

Mbeya City ambayo ilikuwa ikishika mkia, imefikisha pointi nane kutokana na ushindi huo ambapo bao pekee liliwekwa wavuni ni Deus Kaseke katika dakika ya tatu.
Ndanda FC

Ikicheza mbele ya mashabiki wachache huku uwanja ukiwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea mkoani hapa, Mbeya City ilifanya mashambulizi kadhaa huku ikimtumia beki wake mpya klabuni hapo, Juma Nyosso.

Mchezo huo almanusura uahirishwe kutokana na uwanja kuonekana umejaa maji, lakini baada ya mazungumzo mechi ikaendelea kama kawaida.

0 comments:

Post a Comment