Owino amejikuta akianzia benchi katika mechi mbili muhimu, dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe 2, kabla juzi Ijumaa kuachwa kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambapo Simba ilikufa bao 1-0.

Phiri amesema, :“Sina tatizo lolote na Owino na wala siyo kwamba anaumwa, ukiangalia safu yetu ya ulinzi wa kati ina watu watatu, lakini Juuko (Murushid),anahitaji kupata mechi nyingi ili apate uzoefu wa ligi, pia bado naangalia kama kombinesheni yake na Isihaka inaweza kukaa vizuri hivyo ni vizuri akicheza sana.”
Nyota ya Owino iling’ara msimu uliopita akiwa pacha ya Mkenya, Donald Musoti, ambaye hata hivyo alienguliwa, pengo lililotajwa kuitafuna Simba mpaka sasa.

0 comments:
Post a Comment