![]() |
| Pierre Kwizera |
Mrundi huyo alitemwa pamoja na mshambuliaji wa, Amissi Tambwe aliyetua Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Jangwani.Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya kamati ya utendaji ya timu hiyo, kiungo huyo hatalipwa fedha za kusitishiwa mkataba wake ambazo ni milioni 10 na badala watampeleka kucheza soka Oman.
“Tupo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na moja ya klabu ya Oman tutakayompeleka Kwizera tutakayoitaja mara baada ya kukamalisha taratibu zote.“Mara tutakapokamilisha mipango hiyo, basi tutampeleka ili kuepuka gharama tutakazozitumia kumlipa katika kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu.
“Fedha tumepanga kumlipa Tambwe pekee ambaye tuliusitisha mkataba wake kabla ya kwenda Yanga, kikubwa tunataka kumalizana na wachezaji hao kwa amani,”kilisema chanzo hicho.

0 comments:
Post a Comment