![]() |
| Mtibwa Sugar. |
Mchezo huo ulilazimika kuchezwa tena jana saa 2:00 asubuhi, baada ya kuvunjika juzi katika dakika ya nane kipindi cha kwanza kutokana na mvua kubwa iliyonyesha huku timu hizo zikiwa bado hazijafungana.
Katika mchezo huo uliokuwa na kasi kubwa kwa muda wote, Stand ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Shaban Kondo katika dakika ya 22, wakati Said Mkopi iliisawazishia Mtibwa katika dakika ya 86.
![]() |
| Stand United. |
“Mechi ilikuwa ngumu kwani wapinzani wetu (Stand United) nao walicheza vizuri,” alisema Maxime.
Naye kocha wa Stand, Mathias Lule, alisema vijana wake walicheza vizuri na anashukuru kupata pointi moja katika mchezo huo wa ugenini.
“Tumecheza vizuri katika kila idara na Mtibwa nao wakiwa nyumbani wamecheza vizuri pia ndiyo mpira ulivyo tunashukuru kuambulia pointi moja,” alisema.


0 comments:
Post a Comment