COUTINHO SAFARI INAONEKA YANGA.

12/29/2014 02:49:00 pm


KWA mara ya kwanza, kiungo Mbrazili, Andrey Coutinho, ameonja joto la jiwe kwa kutupwa nje ya kikosi cha kwanza, baada ya jana kocha mpya, Hans der van Pluijm kumpiga benchi mwanzo-mwisho.

Coutinho alikuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 18 walioitwa katika mchezo wa jana wakati Yanga ikichuana na Azam uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2, lakini aliishia benchi, ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kufanyiwa hivyo tangu ajiunga na timu hiyo akiwa fiti kiafya.


Katika mechi za awali za Yanga, Mbrazili huyo hakuwahi kuanzia benchi zaidi ya kupumzishwa enzi za utawala wa Mbrazili mwenzake, Marcio Maximo, lakini jana alionja utamu wa benchi.Hata hivyo, huenda yakawa maisha yake mapya kutokana na mfumo wa Mholanzi huyo.

0 comments:

Post a Comment