PLUIJM AMKUMBUKA HAMISI KIIZA.

12/29/2014 01:08:00 pm
Kiiza Hamis
Pluijm Kocha Yanga.

 SIKU chache baada ya kocha mpya wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kukabidhiwa mikoba ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa Mbrazili, Marcio Maximo, amesema kuwa atamkumbuka sana aliyekuwa mshambuliaji wake tegemeo msimu uliopita, Mganda, Hamis Kiiza.

Uongozi wa Yanga hivi karibuni ulimfungashia virago Kiiza na nafasi yake ikachukuliwa na Mliberia, Kpah Sheman ambaye ataitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka miwili.

Pluijm alisema kuwa  baada ya kupata taarifa za Yanga kumtema Kiiza, alisikitika kwani Kiiza alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho.

Pia amesema anaamini  katika hawa wachezaji waliopo hivi sasa Yanga, wapo watakaoiziba vilivyo nafasi ya Kiiza lakini nitamkumbuka sana, alisema Pluijm.Baada ya kutemwa Kiiza alirudi kwao Uganda.

0 comments:

Post a Comment