KESSY: APANIA KUCHEZA KIKOSI CHA KWANZA SIMBA.

12/21/2014 09:22:00 pm
BEKI mpya wa Simba, Ramadhan Kessy, amefunguka kuwa amejipanga ipasavyo katika kikosi hicho kuhakikisha anapata namba kwenye kikosi cha kwanza huku akichekelea kuwa amepata nafasi ya kujiuza kimataifa.

Kessy ametua Simba katika usajili wa dirisha dogo baada ya kuwindwa kwa muda mrefu na klabu hiyo ambapo ametua kwa kubadilishana na mchezaji Miraji Adam.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kessy alifunguka kuwa, ametua Simba kwa kazi moja tu kwani amejiandaa ipasavyo kukabiliana na ushindani wa namba na kudai kuwa hahofii kukutana na washambuliaji mahiri kama aliyetua Yanga, Amissi Tambwe.

Aliongeza amejiunga na Simba kwa kuwa anatambua kuwa itakuwa njia sahihi ya yeye kujiuza kimataifa zaidi na anaona kama ndoto zake zimekamilika.“Nimefurahi kutua Simba, naamini nitafanya vyema kwani kiwango changu nakiamini na nimejiandaa vyema kuhakikisha nakabiliana na ushindani wa namba uliopo katika kikosi hicho.

“Ndoto zangu ni kucheza soka la kimataifa na si vinginevyo. Naamini kusajiliwa na Simba ni moja ya hatua katika ndoto zangu na itakuwa taa ya mafanikio hayo, hivyo sijutii kujiunga nao,” alisema Kessy anayecheza beki ya kulia.

0 comments:

Post a Comment