KOCHA: DIDA AIGHARIMU YANGA.

12/29/2014 03:29:00 pm
Deogratius Munishi, Kipa Yanga SC.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, jana alijikuta akishindwa kujizuia na kumfokea kipa wake, Deogratius Munishi ‘Dida’ kwa madai kuwa alifanya uzembe na kushindwa kuzuia mpira wa kichwa uliopigwa na John Bocco ambao ulizama nyavuni na kuzima ndoto za Yanga kuondoka na ushindi.

Yanga na Azam ziliumana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Bocco ambaye aliingia dakika ya 64 akichukua nafasi ya Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, alifanikiwa kufunga bao la kusawazisha dakika ya 65 akiunganisha krosi iliyopigwa na Himid Mao.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Pluijm alionekana akimfokea Dida kwenye benchi akimtuhumu hakuwa makini golini na kusababisha hadi Bocco kufunga.

0 comments:

Post a Comment