WACHEZAJI SIMBA WAJAZWA MAMILIONI

12/22/2014 12:04:00 pm
Simba SC mabingwa mtani jembe 2014.
USHINDI wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Yanga kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa Desemba 13, mwaka huu umejaza fedha mastaa wa Simba.Katika mechi hiyo, mabao ya Simba yalifungwa na kiungo mshambuliaji, Awadhi Juma na mshambuliaji mwenye umbo kubwa na nguvu nyingi, Elias Maguli.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo, ushindi huo umepokewa vizuri na viongozi ambao wameamua kutoa posho kubwa ya Sh milioni mbili kwa kila mchezaji aliyecheza na Sh milioni moja kwa kila aliyekuwa benchi.

Chanzo hicho kilisema, fedha hizo zimegawanywa kimakundi ambazo ziliwahushisha wachezaji waliocheza katika mechi hiyo na waliokaa benchi.“Kutokana na bidii, kujituma kwa wachezaji katika mechi dhidi ya Yanga ambayo ilimalizika kwa kuwafunga wapinzani wetu mabao 2-0, uongozi umeshawishika kuwapa posho wachezaji wetu.

“Fedha hizo zimegawiwa kwa makundi ambapo shilingi milioni mbili alipewa kila mchezaji aliyecheza mechi hiyo huku wale waliokaa benchi wakipewa shilingi milioni moja kila mmoja.

“Fedha hizo zimetofautishwa ili wachezaji wengine wajibidiishe ili waingie katika kikosi cha kwanza cha kocha wetu Phiri (Patrick),” kilisema chanzo kamili. 

0 comments:

Post a Comment