Simba iliicharaza Yanga mabao 2-0, hali iliyosababisha kuvunjwa kwa benchi la ufundi lililokuwa chini ya Mbrazili, Marcio Maximo.Akizungumza na Championi Jumatatu, Phiri alisema kuwa hakuamini kama matokeo yale yangetokea.
“Yalikuwa ni matokeo ya kushangaza kidogo, lakini ndiyo mpira ulivyo. Tulicheza vyema, tulimiliki mpira lakini ajabu tulishindwa kupata ushindi.
“Siwezi kumlaumu mchezaji mmojammoja, lakini chanzo naona kilikuwa ni kujiamini kupita kiasi baada ya kupata matokeo mazuri mechi tatu nyuma. Tulifanya vyema dhidi ya Yanga, tukashinda tena dhidi ya Mwadui, hata kule Zanzibar tulishinda, kwa hiyo walijiamini sana wakadhani mechi ingekuwa rahisi.
“Ndiyo maana walikuja kushtuka zaidi kipindi cha pili kutafuta bao la kusawazisha, lakini haikuwa rahisi kutokana na mbinu mbovu waliyotimua Kagera ya kupoteza muda,” alisema Phiri.
Hata hivyo, alipoulizwa maoni yake juu ya bao jepesi alilofungwa kipa wake Ivo Mapunda alisema:
“Ni kweli ulikuwa ni uzembe, lakini siyo kipindi cha kulaumiana, kama ni kosa alifanya kosa kama makipa wengine, lakini tusisahau hatari nyingine alizoweza kuokoa, kwa hiyo siwezi kukubaliana na wanaomlaumu kiasi hicho.”

0 comments:
Post a Comment